|
Shule ya sekondari ya Ruhuwiko ipo kwa mujibu wa sheria na inafuata taratibu zote za kuwasajili wanafunzi kujiunga na shule kama zilivyowekwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Ufuatao ni utaratibu na sifa zitumikazo katika ofisi ya usajili kuwasajili wanafunzi kujiunga na shule. |
1. Kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza.
- Awe na umri wa miaka 13 hadi 16.
- Awe amemaliza darasa la saba.
- Awe anajua kusoma na kuandika.
- Kabla ya kujiunga mwanafunzi anatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga
- Awe na kivuli cha cheti cha kumaliza darasa la saba au barua ya uthibitisho toka kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi aliyosoma.
- Awe na kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
|
2. Kwa wanafunzi wa kidato cha tano.
- Anatakiwa awe amemaliza kidato cha nne na kupata angalau ufaulu wa "C" tatu na kuendelea.
- Awe na kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Awe na kivuli cha cheti cha kumaliza kidato cha nne au kivuli cha cheti cha matokeo kidato cha nne.
|
3. Kwa Wanafunzi wa kuhamia.
- Kabla ya kujiunga na shule anatakiwa kufanya mtihani wa kuhamia na anatakiwa kufaulu kwa kiwango kilichowekwa na shule.
- Lazima alete uhamisho toka shule aliyotoka kabla ya kusajiliwa.
- Kwa mwanafunzi anayehamia kidato cha kwanza hadi cha nne awe na kivuli cha cheti cha kuzaliwa na kivuli cha cheti cha darasa la saba au barua ya uthibitisho toka kwa mwalimu mkuu.
- Kwa mwanafunzi anayehamia kidato cha tatu na cha nne aje na matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili.
- Kukariri darasa ni lazima mwanafunzi apate kibali toka kwa afisa elimu mkoa ndipo ataruhusiwa kukariri.
|
ZINGATIA: Wanafunzi wote wanapokelewa bila ubaguzi wa aina yoyote ilimradi awe amekidhi vigezo vinavyotakiwa.
|